September 8, 2022

Uncategorized

KCSE Past Papers 2016 Kiswahili Paper 3 (102/3)

Kenya Certificate of Secondary Education 2016 Kiswahili Karatasi ya 3 Lugha SEHEMU A: HADITHI FUPI K. Walibora na S. A. Mohamed: Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine 1. Lazima Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa “Kanda la Usufi”, “Shaka ya Mambo” na “Tazama na Mauti”. (Alama 20) SEHEMU B: RIWAYA K. Walibora: Kidagaa Kimemwozea Jibu swali la 2 au la 3 2. Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya: Kidagaa Kimemwozea. (Mama 20) 3. “Wasemao husema, atafutaye hachoki.” (a) Fafanua muktadha wa dondoo hill. (Alama 4) (b) Kauli hii ina maana gani kwa mujibu wa muktadha huu. (Alama 2) (c) Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (Alama 14) SEHEMU C: TAMTHILIA T. Arege: Mstahiki Meya Jibu swali la 4 au la 5 4. “Anwani Mstahiki Meya ni kinaya.” Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia. (Alama 20) 5. “…dawa ya adui ni kummegea unachokula.” (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4) (b) Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa Cheneo. (Alama 16) SEHEMU D: USHAIRI Jibu swali la 6 au la 7 6. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Kilio cha Lugha Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi Kiwa kwetu naumia, kwcngine si mahususi Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia. Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa Hamna nami imani, wala kupanga siasa, Mwasema sayansini, siku ningalitosa, Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika. Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu, Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu, Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu, Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia. Mzaliwapo mwalia, `maa’, maneno ya kwanza, Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza, Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza, Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza. Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza, Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza, Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza, Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia? Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao, Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa. Enyi viongozi wetu ipangeni nadharia, Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria Lugha hata `mbusha watu, tuche kuriaria, Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia. Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote, Msamiati huwa, ni wa Afrika yote, Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote, Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika. Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi, Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi, Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi Kwao `meomba kiasi, iii kujizidisha. Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya, Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya, Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya, Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia. Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana, Kukua imeridhia, msamiati kufana, Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana, Lugha yenu ya maana, mwaipuuza yalia. (a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu. (Alama 2) (b) Kwa kutoa hoja nne, eleza kwa nini shairi hill likaitwa kilio cha lugha. (Alama 4) (c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (Alama 4) (d) Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2) (e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatn. (Alama 3) (f) Bainisha nafsineni katika shairi. (Alama 2) (g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi. (Alama 3) (i) nasongwa (ii) kuriaria (iii) adinasi 7. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Barabara Barabara bado ni ndefu Nami tayari nimechoka tiki Natamani kuketi Ninyooshe misuli Nituliza akili. Lakini Azma yanisukuma Mbele ikinihimiza kuendelea Baada ya miinuko na kuruba Sasa naona unyoofu wake Unyoofu ambao unatisha zaidi. Punde natumbukia katika shimo Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena Ghafla nakumbuka ilivyosema Ile sauti zamani kidogo “Kuwa tayari kupanda na kushuka.” Ingawa nimechoka Jambo moja li dhabiri Lazima nifuate barabara Ingawa machweo yaingia Nizame na kuibuka Nipande na kushuka. Jambo moja nakukumbukia: Mungu Je, nimwombe tena? Hadi lini? Labda amechoshwa na ombaomba zangu Nashangaa tena! Kitu kimoja nakiamini Lazima niendelee kijitahidi kwa kila hatua mpya Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu Nikinaswa na kujinasua Yumkini nitafika mwisho wake Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla. (a) Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2) (b) Tambua nafsineni katika shairi hili. (Alama 2) (c) Mshairi ana maana gani anaposema “Kuwa tayari kupanda na kushuka” katika ubeti . wa tatu? (Alama 2) (d) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili ukizitolea mifano mwafaka. (Alama 10) (e) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili. (Alama 2) (f) Eleza maana ya: (i) kuruba (ii) barabara yenye ukungu (Alama 2) SEHEMU: FASIHI SIMULIZI 8. (a) Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii. (Alama 10) (b) Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji. (Alama 10)    

KCSE Past Papers 2016 Kiswahili Paper 3 (102/3) Read Post »

Uncategorized

KCSE Past Papers 2016 Kiswahili Paper 2 (102/2)

Kenya Certificate of Secondary Education 2016 Kiswahili Karatasi ya 1 Lugha 1 UFAHAMU: (Alama 15) Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Ulimwengu unatakiwa kuzua mbinu za kulitatua tatizo la ufukara ambao ni kikwazo kikuu cha juhudi za maendeleo. Ufukara unayakabili mataifa mengi yanayoendelea na kuyatosa kwenye shida nyingi huku mataifa ya magharibi yakizidi kupiga hatua kubwa za kimaendeleo. Tofauti iliyopo kati ya mataifa yanayoendelea na yaliyoendelea inaendelea kuongezeka kila siku. Miongoni mwa sababu zinazochangia katika ufukara huu ni pamoja na ufisadi, uongozi mbaya, turathi za kikoloni na uchumi unaotegemea kilimo ambacho hutegemea mvua isiyoweza kutabirika. Vilevile, mataifa yanayoendelea yana idadi kubwa ya watu inayoupiku uwezo wa mataifa husika. Pamoja na haya, mataifa haya hayana uwezo wa kuwakomboa raia wake kutoka katika lindi la umaskini huu unaokithiri. Ukosefu wa elimu na nafasi adimu za kazi huchangia pia katika tatizo hili. Ni wazi kuwa ufukara una athari hasi kote ulimwenguni. Aghalabu, ufukara huchipuza matendo mabaya. Ni rahisi kuwashawishi wananchi maskini kushiriki katika uhalifu iii kujinasua kutoka kwenye lindi la kimaskini. Udhaifit huu huweza kuzaa mbegu ya kuatika maovu ya kila aina ukiwemo ugaidi. Mataifa yaliyoendelea yanatakiwa kuyaburai madeni yanayoyadai mataifa yanayaoendelea kama njia moja ya kupambana na ufukara. Mataifa haya maskini hutumia asilimia kubwa ya mapato ya kitaifa kuyalipia madeni haya. Hali hii imeyafanya mataifa haya kushindwa kujikwamua kutoka kwenye minyororo ya ufukara. Njia nyingine ya kuyasaidia mataifa haya ni kukubali kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi husika. Mataifa yanayoendelea nayo yanatakiwa kuchukua hatua katika kuwanusuru raia wake kutoka kwenye dhiki hii. Ni sharti yaibuke na mikakati kabambe ya kupambana na ufukara. Itakuwa na faida kubwa iwapo mataifa haya yataunda sera zinazotambua ufukara kama tatizo kuu linalozikabili na kuweka mikakati ya kuwaokoa raia wake kutoka kwenye tatizo hili. Pamoja na mikakati hii ni kuzalisha nafasi za kazi, kuimarisha miundo msingi, kuendeleza elimu inayolenga kutatua matatizo maalumu katika jamii na kupanua viwanda. Kuna pia haja ya viongozi kuwa waangalifu iii mfumo wa soko huru ambao unaendelezwa na mataifa yaliyondelea usiishie kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia. Maamuzi yote ya sera za kiuchumi sharti yauzingatie uhalisia wa maisha ya raia wa mataifa haya. (a) Eleza athari za madeni kwa nchi zinazoendelea. (alama 1) (b) Kwa nini umaskini unatawala mataifa yanayoendelea? (alama 4) (c) Mwandishi anatoa mapendekezo yapi kwa mataifa yanayoendelea katika kutatua tatizo la ufukakra? (alama 4) (d) Mfumo wa siko huru una mathara gani kwa mataifa yanayoendelea? (alama 2) (e) Taja visawe vya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu. (alama 3) (i) turathi za kikoloni (ii) kuatika (iii) kuyaburai 2 MUHTASARI: (Alama 15) Soma kifungu laluatacho kisha ujibu maswali. Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima sawa. Utaifa hujengwa kwenye misingi ya mapenzi kwa nchi. Utambuzi wa cheo, eneo, hadhi, rangi na hata makabila wanakotoka raia wa taifa moja si chanzo cha kuwatanganisha. Nchi moja huweza kuundwa na watu walio na tofauti chungu nzima zikiwemo tofauti za kikabila, kitabaka na kimawazo. Hata hivyo, watu hawa huwa na kitu mfano wa gundi kinachowaunganisha na kuwafanya kuonea fahari nchi yao. Watu hao huwa na falsafa na imani sawa kama taifa inayoashiriwa hasa na wimbo wa taifa. Hata hivyo haya yote hayawezi kuwafikia katika kiwango cha kuunda taifa. Uzalendo ndio mhimili mkuu wa utaifa. Uzalendo ni mapenzi aliyo nayo mtu kwa nchi yake. Mapenzi haya humwongoza mtu katika mawazo yake, itikadi yake, matendo yake, matamanio yake na mkabala wake kuhusu nchi na hatima ya nchi yake. Mzalendo hawezi kushiriki katika matendo yanayowcza kuiletea nchi yake maangamizo kwa vyovyote vile. Mzalendo huongozwa na mwenge wa wema. Mzalendo hawezi kushiriki kwenye shughuli zozote zinazohujumu mshikamano wa kitaifa. Yeye hatawaliwi na ubinafsi wa kutaka kufaidi nafsi yake na ya jamii yake finyu. Matendo yake yote huongozwa na ari ya kuiboresha nchi yake. Anayeipenda nchi yake hujiepusha na ulafi wa kujilimbikizia mali. Yuko radhi kuhasirika mradi taifa lake linufaike. Utaifa ni mche aali unaopaliliwa kwa uzalendo, kuepuka uchu wa nafsi na taasubi hasi zikuwepo za kikabila na ubinafsi. Hali hii inapofikiwa, hatima ya taifa na mustakabali wa raia wake huwa wenye matumaini makubwa. (a) Kwa maneno 40 — 50 dondoa sifa kuu za utaifa. (alama 6, 1 ya mtiririki Matayarisho Nakala safi (a) Kwa maneno 40 — 50 dondoa sifa kuu za utaifa. (alama 6, 1 ya mtiririki Matayarisho Nakala safi 3 MATUMIZI YA LUGHA: (alama 40) (a) Tumia nomino yoyote katika ngeli ya 1 —1 kutunga sentensi. (alama 1). (b) (i) Nini maana ya silabi. (alama 2) (ii) Tunga neno lenye muundo huu wa silabi: lrabu + konsonanti + konsonanti + irabu. (c) Tunga sentensi hii upya kwa kufuata maagizo: Wasichana wanaingia darasani kwa haraka. (Andika kinyume chake). (alama 2) (d) Tambua kiambishi awali na tamati kati neno: Alalaye (alama 2) (e) Ainisha vivumishi katika sentensi hii. Mzee mwenyewe ni mkongwe na amepewa zawadi kwa kuwa shamba lake lilitoa mazao mengi. (alama 4) (f) Askari wasipopiga doria wala kushirikiana na raia hawatakuwa wametuhakikishia usalama. (yakinisha sentensi hii) (alama 2) (g) “Shughuli yetu itakamilika kesho-., mama alimwambia mwanaye Juma (Andika katika usemi wa taari fa ). (alama 2) (h) Changamua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha matawi. Mpira ulichezwa tulipokuwa tukipika. (alama 3) (i) Dhihirisha matumizi matatu tofauti ya kimaana yatakayotokea kitenzi “ona” kikinyambuliwa katika kirai hiki “ona ndoto”. (alama 3) (j) Eleza matumizi ya hali za “ka” na “hu” katika sentensi zifuatazo: (i) Balozi huja Napa kila mara. (Attila 1) (ii) Mpishi alipika, *us mkuwa na ak%gawa chakula. (alama 1) (k) Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi: Tuliitwa na baba. (alama 2) (1) Akifisha: Shangazi alimwambia mwanawe njoo nikupeleke kwenu jioni motto aliuliza kwetu wapi? (alama 4) (m) Eleza matumizi mawili ya kiambishi —ji- (alama 2) (i) (n) Tunga sentensi hii upya kwa kutumia visawe vya maneno yaliyopigwa mstari. (alama 3) Kiambaza kilimuumiza ghulamu alipokuwa akipanda. (o) Tumia kitenzi “Fa” katika sentensi kuonyesha mazoea. (alama 2) (p) Ainisha vihusishi katika sentensi ifuatayo: Babu alifika mapema kuliko wote halafu akaondoka. (alama 2) (q) Tumia kitenzi “tafakari” kama nomino katika sentensi. (alama 1) (r) Andika

KCSE Past Papers 2016 Kiswahili Paper 2 (102/2) Read Post »

Uncategorized

KCSE Past Papers 2016 Kiswahili Paper 1 (102/1)

Kenya Certificate of Secondary Education 2016 Kiswahili Karatasi ya 1 Lugha 1 Lazima Wewe ni katibu wa kamati inayochunguza jinni ya kupambana na tatizo sugu la dawa za kulevya. Andika ripoti ukitoa mapendekezo ya kamati. 2 “Utalii una faida nyingi kuliko madhara nchini Kenya.” Jadili. 3 Andika insha inayobainisha maana ya methali’: Chombo cha kuzama hakina usukani. 4 Tunga kisa kitakachomalizika kwa: “Niligugumia ile chupa ya maji kwa pupa. Sikuamini kuwa kiu yangu ingekatika. Baada ya kumaliza kunywa maji yote, ndipo nilipotambua kwa kweli kuwa maji ni uhai.  

KCSE Past Papers 2016 Kiswahili Paper 1 (102/1) Read Post »

Uncategorized

KCSE Past Papers 2017 Kiswahili Paper 3 (102/3)

Kenya Certificate of Secondary Education 2017 Fasihi Karatasi ya 3 Sehemu A: Fasihi Simulizi Lazima (20 marks) Sama utungo ufuatao kisha ujibu maswali. Walikuja mahasidi, ah, walikuja Nyayo zao zikirindima, ah rindima Kwa ghamidha ya uadui, 00 uadui Wali Wakibeba sime Wali wakibeba mata Wali Wakibeba mienge ya moto kutangazia kwao kuwasili Walikuja kwa ndimi zilohimili cheche matusi kutumwaiya. Hawakuj ua ya kwamba mbele ya mhimili huno wetu wao wali vipora. Kwenye Mlima wa Sugu, walituvamia. Aliwakabili Mbwene Mwana wa Ngwamba, ee Mbwene Aliwakabili Mbwene kwa kitali kikali. Wali wametuteka ja samaki kwenye dema Wali wamewapukutisha wetu mabarobaro Aliwakabili Mbwene Ee Mbwene, Mwana Wa Ngwamba Aliwakabili kwa hamasa za ujana kwa uchungu wa kuumbuliwa wa wetu wana. Aliwakabili Mbwene Nao wakalipiza shambulizi kwa kujidai majagina walijibwaga uwanjani Laiti wangalijua wanajikabidhi viganjani mwa Mbwene. Aliwakabili Mbwene, ee Mwana wa Ngwamba, shujaa asoshindwa alipigana kitali cha kufa na kupona kuiopoa jamii yetu, kuirejesha hadhi yetu. kuirejesha mifugo yetu kuwarejeshea wakulima vikataa vyao kuwaokoa vipusa wetu nyara Waliotekwa, ati Walipiza kisasi. Aliwakabili Mwana Wa Ngwamba Aliwakabili Upepo Wa Kusi Hata kikorno cha mapambano kilipofika Wagundi walijua kwamba Walikuwa na Mwana, ee Mwana Mbwene, ee Mwana wa Ngwamba Hakuwa na kifani, ee kifani Alipigana nao, cc Mwana wa N gwamba Kwa siku kumi bila tonge wala tone la maji Kwetu kukenda kicheko cha Wokovu Kwao kukenda kilio. (a) “Huu ni wimbo wa sifa.” Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano mitatu kutoka kwenye utungo huu. (alama 3) (b) Andika sifa tatu za jamii ya nafsineni katika utungo huu. (alama 3) (c) Huku ukitoa mifano, bainisha vipengele vinane vya kimtindo ambapo nafsineni imetumiwa kufanikisha uwasilishaji wa umngo huu. (alama 8) (d) Tungo za aina hii zinaendelea kufifia katika jamii yako. Fafanua hoja sita utakazotumia kuishawishi jamii yako kukinga dhidi ya hali hii. (alama 6) SEHEMU B: RIWAYA K. Walibora: Kidagaa Kimemwozea Jibu swali la 2 au la 3. 2. “Lakjni waliogopamwaliogopa hata kuwa na uoga.” (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) (b) Bainisha tamathali lnoja ya usemi ambayo imetumiwa katika dondoo hili. (alama 2) (c) Kwa kurejelea hoja kumi na nne kutoka kwenye riwaya hii, thibitisha kwamba raia wa Tornoko walistahili kuogopa hata kuwa na uoga‘ (alama 14) 3. (a) “Usinivue nguo kwa macho yako wee!” Kwa kurejelea hoja kumi na mbili kutoka kwenyc riwaya hii, thibitisha kwamba mzungumzaji anastahili kuvuliwa nguo. (alama 12) (b) Tathmini umuhimu wa barua ya Ben Bella kwa Mashaka katika kuijenga riwaya hii. (alama 8) SEHEMU C: TAMTHILIA T. Arege: Mstahiki Meya Jibu swali la 4 au la 5. 4. “Tuyashughulikie ya leo. Kesho, keshokutwa na mtondo harutakuwepo. Wayatakig nigi ya mtongggoo? ” (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) (b) Bainisha sifa ya rnzungumzaji inayodokezwa na kauli iliyopigiwa mstari. (alama 1) (c) Eleza sifa tano Za anayeambiwa maneno haya. (alama 5) (d) Kwa kurejelea hoja kumi kutoka kwenye tamthilia, onyesha jillsi kutoyataka ya mtondogoo kulivyozorotesha hali ya maisha Cheneo. (alama 10) 5. “Ni mgao Wa wakubwa kula kwanza na sisi wengine kupigania makombo yanayoanguka chini.” (a) Fafanua sifa tano za rnzungumzaji. (alama 5) (b) Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hoja kumi na tano kutoka kwenye tamthilia. (alama 15) SEHEMU D: USHAIRI Jibu swali la 6 au la 7. 6. Soma shairi lzfuatalo kisha ujibu maswali. Mwanangu, Wenye dhambi vishawishi, vikejeli Mwanangu, katu wasikushawishi, binkuli Mwanangu, aushi nayo uishi, kama mwali Mwanangu sikubali! Mwanangu, sherati sikuperembc, kakubali Mwanangu, usiwache wakubembe, kwa sali, Mwanangu, mithili yao mapembe, ya fahali Mwanangu sikubali! Mwanangu, wajeuri siwe nao, ni shubili Mwanangu usifwate njia zao, pita mbali Mwanangu, ujeuri scra yao, mazohali, Mwanangu sikubali! Mwanangu, Waongo usiwasifu, kulihali Mwanangu, uongo ubatilifu, si amali Mwanangu, ndimi zao hazikifu, si manzili Mwanangu sikubali! Mwanangu, wafisadi siwe nao, kemikali Mwanangu, tamaa ndo utu wao, si Injili Mwanangu, Wahepe kila uchao, kiakili Mwanangu sikubali! Mwanangu, wote walio wabaya, Wanadhili Mwanangu, usije ukawapeya, ikibali Mwanangu, katika hino duniya, kaa mbali Mwanangu sikubali! (J. Kiponda) ( a) Fafanua mambo sita ambayo yanaweza kuzorotesha maadili ya anayelengwa na shairi hili. (b) Bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumiwa katika shairi hili. (c) Andika aina mbili za urudiaji zilizotumiwa katika shain’ hili. (d) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyoz (i) idadi ya vipande katika mishororo. (ii) mpangilio wa maneno katika mishororo (m) idadi ya mizani katika mishororo. (iv) mpangilio wa vina katika beti. (e) Andika aina mbili za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika shairi hili. if I Andika ubeti wa tano kwa lugha ya nathari. Soma Shairi Iifizatalo kisha ujibu maswali. Walo nacho hawachi mshangao kunitia Moyoni watakutia pindi waonapo we u chambo cha kuvutia rasilimali huko kwenye vina Hawachi kukwinamisha kukupindisha mgongo ndoana urneshika kuvulia yao riziki. Watakwita kwa majina ya hadhi ya kupembeja ya kukwaminisha kwamba We na wao mu Wamoja hali zenu kama sahani na kawa wanakwonyesha wao nawe mwachumia jungu moja yenu matarajio ni mamoja Watakwahidi halua kila tunu watakwashiria mradi nyoyo zao zimemaizi We u nundu ya kukamulia mafuta we u ndovu wa mti kugonga makoma kuangusha wafaidi wao. Mabepari wana mambo ukiwa yao makasia ya kuliendesha dau lao majini lielee miamba kulepusha Watakusifil Watakuchajiisha mbele utunge machoyo yenye ari huku wanakufunga nira ja fahali mali kuwazalishia huku kipato wakupimia kwa kibaba usipate kukidhi haja usipate kujarnini kuwategemea uzidi. Hawa ni wa kuajabiwa Watakupa yao kazi Mpangilio wa kazi wakukabidhi Wao na malengo wakupe La! Hawakupi! Wanakuhusisha katika kuyavyaza na muda wa kuyafikia nao mwaafikiana ati kuna makubaliano bayana ambayo ubatizo Wayo ni kandarasi ya utcndakazi. Ela We nao mnajua ndo kigezo cha kupimiamWako uwaj ibikaji wako mchango chunguni yako thamani Na usidhani una hiari ya kuamua tapofika Watakusukuma lmfikia yao shabaha bila lmwazia ujixa wanokupa. Watakuhimiza kuturnia chako kipawa kuikoza nundu yao mafuta Viumbe hawa! Mabepari – waajiri (a) Eleza mikakati sita inayotumiwa na waajiri kujikuza kiuchumi. (alama 6) (b) Bainisha tamathali tatu za usemi zilizoturniwa katika shairi hili. (alama 3) (c) Huku ukitoa mifano, bainisha aina mbili za uhum wa kishairi aliotumia mshairi. (d) Andika mifano ya mistari mishata katika shairi hili. (6) Bainisha nafsineni katika shairi hili. (f) Fafanua toni

KCSE Past Papers 2017 Kiswahili Paper 3 (102/3) Read Post »

Uncategorized

KCSE Past Papers 2017 Kiswahili Paper 2 (102/2)

Kenya Certificate of Secondary Education 2017 Kiswahili Karatasi ya 2 Lugha UFAHAMU: (Alama 15) Soma kifimgu kifilatacho kisha ujibu maswali. “Asante baba, asante mama,” akasema Bahati jioni moja baada ya chajio, “Sijui ilitokeaje kukawa na Waru Wanaothamini binadamu Wenye mahitaji maalumu katika jamii hii. Sitawauliza mlichofanya kunikinga na hukumu ya ukoo ya kuniangamiza; hayo mtakuja kunihadithia siku rnoja. Ila nataka rnjue kwamba khishi na ulemavu Wa aina yoyote ile kuna dhiki kuu. Niliyokabiliana nayo baada ya uamuzi wenu wa kunipeleka shuleni hayawezi kutoshea hata chapisho la kurasa elfu. Si kudhihakiwa na miale ya jua; ngozi yangu inashindwa kuuhimili ukali wake, si kutengwa na marika, si kulazimika kusoma hati za kawaida hadi pale serikali ilipoanzisha sera ya kuhakikisha kwamba matini zote za kiusomi zimeandikwa pia kwa hati ambazo zinaweza kusomwa na Wenye changamoto kama yangu, si kubaguliwa kazini….” Bahati alitua, akawatazama wazazi wake kama anayetaka kuona taathira ya maneno yake kisha akaendalea. “Msinione kama aliyckosa hisani, ila’ nataka niwaambie kwamba hata uamuzi wenu wa kunitafutia mlinzi kuandamana nami hadi shuleni ulinitia kwenye ngome zaidi. Nilijihisi kama niliyedhulumiwa zaidi katika kule kulindwa! Najua mlikuwa mnachelea kwamba ningekuwa windo rahisi kwa walanguzi wa binadamu ambao wanaamini kwamba viungo vyetu sisi ni dawa ya kutibia ndwele mbalimbali. Hata hivyo, katika kipindi chote hicho nilitamani kwamba mngcnifimza mbinu za kujilinda mimi binafsi. Amini usiamini hata nilitamani kwamba ningetekwa nyara, nijadiliane na Watesi wangu kuliko kupokwa nafasi ya kubuni mikakati ya kujihakikishia usalama”. “Mwanangu Bahati,” alisema mume wangu, “binadamu hawi jagina kwa kuzifimta tamaduni za jamii yake bila kuzichunguza. :haidhuru kwamba ilichukua muda kuyangamua haya’. La muhimu ni kwamba umeweza kuishi kama ndugu zako”. Nilimtazama mume wangu kwa macho yaliyokuwa yamepofushwa na dimbwi la machozi. Moyo uliituma akili yangu kurudi nyuma kule -e-e-e- kwenye miereka ya baada ya kuzaliwa kwa Bahati. Asubuhi hiyo ya kipupwe nilishika ujia ulioelekea kwenye msitu uliokuwa karibu na boma la Mzee Kedi, baba mkwe wangu; mgongoni nimeifungia mbeleko ambayo ilikisitiri kitoto changu. Nilitazama nyuma, nikaiona nyumba ambayo mimi na mume wangu tulikuwa tumechanga bia kuijenga. “Haya yote nayaacha,” nilijiambia, “nayaacha na mengine mengi. Nawaacha mabinti wangu wawili, namwacha mume wangu, naiacha kazi yangu, nayaacha rnaisha yangm Wala sijuti kwa kuyaacha haya yote. Sina cha kujutia kwani imebidi kuondoka. Jamii yangu imenitema; mimi na mwanangu. Haina nafasi ya mwanangu, kwa hivyo nami nimeamua kwamba haina nafasi yangu kwa vile imesema huu ni mzigo wangu. Ikiwa ukoo umeamua kuwa hatima ya mwanangu huyu ni kuwa kitoweo cha fisi, basi na tuwe sote karamu ya fisi,” nilitamatisha kauli yangu kisha nikayarudisha nyuma tena mawazo yangu. Nilikumbuka sauti ya muuguzi hospitalini siku ambayo nilijikopoa, “Pongezi Tamasha, Mungu amekutunukia kipusa”. Nilikifunua kitoto changu kilichokuwa kimefunikwa gubigubi, nikakitazama viguu, vikono, uso…kisha, ‘Mungu wangu!’ ikanitoka. “Dadangu, unastahili kumshukuru Mungu,” akasema rnuuguzi, “wapo wanawake, mimi mwenycwe nikiwemo, ambao hawajawahi kuambulia uj auzito, sikwambii hata kupoteza mimba. Huyu wako ni kiumbe kamili, kasoro yake i kwenye ngozi tu, na hii ni hali ambayo unaweza kukabiliana nayo. Hapa lmionapo nimelazimika kumpa mume wangu talaka, mwenyewe alienda kortini akaiomba. Anadai kwamba hatusikilizani. Ila najua kiini cha haya yote ni kutoshika kizazi”. Nilimtazama huyo muuguzi kana kwamba hajaserna lolote. Nilimwona kama anayeuona mzigo wangu kuwa kanda la usufi. Huenda huyu muuguzi hakujua kwamba katika jamii yangu watoto wa aina hii ni kama pacha, huaminiwa kuwa nuksi kwa ukoo mzima, kwa hivyo hutupwa. Muuguzi huyu hakujua pia kwamba tayari nilikuwa na watoto wawili wa kike na huo tayari ulikuwa mzigo mkubwa kwaugu kwani ilibidi kumhakikishia mavyaa kila mara kwamba hawa pia walikuwa watoto. Moyo ulinipa kukumbuka jitimai iliyojiandika usoni mwa mume wangu asubuhi hiyo alipokuja hospitalini. Alikitamma lcitoto chetu kana kwamba anaona mzuka. Alinyamaza kwa muda, akashusha pumzi, kisha akanishika kwenye bega na kuondoka kwenyc wodi. Machozi yalivunja kingo zake huko yanakohifiadhivya, nikalia kama mfiwa, Mume wangu alirudi tena baada ya siku mbili; anakuja kunipcleka nyumbani. “Mke wangu, naomba msamaha kwa kutokuja kuwatazama kwa siku mbili. Ilibidi nishauriane 11a ukoo kuhusu lnnzia Inavyoonekana ni kwamba msimamo wa baba na wazee wenginc ni ule ule. Wanasema ukoo wa Baulanga haujawahi kupata mtoto wa aina hii, kwarnba kumhifadhi mwana huyu kumkuwa kuupaka masizi ukoo. Wahenga hawatakubali tendo hili. Sijui nitakutetea vipi. Nimo kwenye njia panda,” mume wangu alikamlisha uzungumzi wake na kuelekea kwenye afisi ya mhasflm kukamilisha w’viga vya kutuondoa hospitalinj. “Huna haja ya klmitetea. Sijafanya kosa lolote. Nililofanya ni kujaliwa kiumbe ambaye anaonekana kuwa punguani kwa misingi ya jamii yako. Nitakilinda kitoto hiki hata kifoni,” nilimwambia mume wangu mawazoni. (a) “Kufauikiwa kwa watu wenye mahitaji maalumu ktmategemea jamii.” Thibitisha kwa kutoa hoja sita kutoka aya tatu za kwanza. (alama 6) (b) Kwa kurejelea aya ya nne hadi ya saba, onyesha jinsi unyanyasaji Wa kijinsia unavyoendelezwa katika jamii hii. (alama 3) (c) “Msimulizi anahimiza. uwajibikaji.” Thibitisha kwa kutoa hoja nne kutoka aya tatu za ‘ mwisho. (alama 4) (d) (i) Andika kisawe cha, ‘hisani’ kwa mujibu wa taarifa. (alama 1) (ii) Elcza maana ya, ‘kuupaka masizi’ kulingana na taarifa. (alama 1) 2. UFUPISHO: (Alama 15) Soma kifimgu kifitatacho kisha ujibu maswali. Moja kati ya mambo ambayo yarnerahisisha maisha ya binadamu ni maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia. Siku hizi shughuli nyingi ambazo zilichukua muda kutekelezwa zinachukua muda mfupi sana. Tuchukue kwa mfano shughuli za usafiri na utendaji kazi. Siku hizi zipo mashinc ambazo zinafanya kazi kuwa nyepesi mno. Kwa mfano, katika ukulima, kuna mashine za kulima, kuvuna na hata kupura nafaka. Magari nayo yamerahisisha usafili na upashanaji habari. Safari ambayo awali ilichukua siku mbili au tam, siku hizi inachukua siku moja an hata saa chache tu kwa sababu ya kuwepo kwa magari ya kisasa. Katika sekta ya elimu, maendeleo makubwa yameshuhudiwa. Siku hizi mwalimu anaweza kuhuisha some lake kwa kutumia. tarakilishi. Vipindi mbalimbali vimenaswa na kuhifahiwa kwenye kompyuta. Itokeapo kwamba mwalimu wa darasa atakosa kuhudhurj/a somo, wanafunzi wanaweza kufunzwa na mwalimu wa kompyuta. Shughuli za utafiti nazo zirnefaidika mno kutokana na uvumbuzi wa kiteknolojia. Wasomi na wanafunzi wanaweza kupata matini mbalimbali za rejea kupitia kwenyc mtandao. Hili linasaidia kufidia upungufu Wa vitabu vya kikaida. Hali kadhalika, maendeleo ya kiteknolojia yamerahisisha shughuli za usajili vyuoni na hata

KCSE Past Papers 2017 Kiswahili Paper 2 (102/2) Read Post »

Uncategorized

KCSE Past Papers 2017 Kiswahili Paper 1 (102/1)

Kenya Certificate of Secondary Education Kiswahili – Insha 1. Lazima Shirika la kigeni la Tugawane limeanzisha kiwanda cha kutengenezea matofali katika eneobunge Ienu. Mwandikie barua Mhariri wa Gazeti la Mzalendo ukitoa maoni yako kuhusu faida na changamoto zinazoweza kutokana na mradi huu. 2. Andika insha kuhusu umuhimu wa mwanafunzi kujiunga na vyama mbalimbali shuleni._ 3. Tunga kisa kitakachodhihilisha maana ya methali ifuatayo: Papo kwa papo kamba hukata jiwe. 4. Tunga kisa kitakachomalizika kwa maneno yafuatayo: Sikuupa moyo wangu nafasi ya kujutia niliyoyatenda. Nilikuwa nimeamua kuyajenga maisha yangu upya. …………………………………………………………… …………………………………………………………… …………………………………………………………… ……………………………………………………………

KCSE Past Papers 2017 Kiswahili Paper 1 (102/1) Read Post »

Uncategorized

COLLECTION MANAGEMENT NOTES

1.1 Concept of Collection Development The term collection development gained wide application in the late 1960s to replace selection  as a more encompassing term reflecting the process of developing a library collection in response to the missions and priorities of the library or institution being served as well as the community and user needs and interests.  Collection development  involves planning and acquiring a balanced collection of information materials over a period of years, based on an ongoing assessment of the information needs of the information centre’s clientele, analysis of usage statistics and demographic projections.  Broadly speaking, collection  development  covers  several  activities  related  to  the  development  of  library collections  including  selection,  the  determination  and  coordination  of  selection  policy, assessment of the needs of users and potential users, collection use studies, collection analysis, budget management, identification of collection needs, community and user outreach and liaison, and planning for resource sharing. Collection development process involves the following components: Needs analysis – understanding the needs and wants of the library users as well as a profile of who they are. Creation of a collection development policy Selection Acquisition Deselection (Weeding) Evaluation of collection Typically, a library or information centre should develop a detailed plan involving the who, what, when, where, why, and how in the whole collection development process. 1.2 Objectives of Collection Development Collection development is primarily concerned with providing the library or information centre with information resource that meet both the actual and anticipated needs of its clients. These needs may not be static; rather they change with the environment. This dynamism of user  information  needs  compels  information  centres  to  review  collection  development activities from time to time to accommodate emerging needs. In order for a library or information centre to achieve its mission, each segment of the collection must be developed keeping in mind its relative importance to the mission of the parent institution as well as the needs of its users. 1.3 Principles of Collection Development The process of collection development is usually guided by a written collection development policy. A collection development policy is a document which defines the scope of an information centre’s existing collections, plans for the continuing development of resources, identifies collection strengths and outlines the relationship between selection philosophy and the institution’s goals. It is considered as one of the first pieces of evidence in determining whether an information centre is engaged in good collection development practices. A collection development policy guides activities related to planning, budgeting, selecting and acquiring of information materials Collection development policy informs everyone about the nature and scope of the collection and collecting priorities. It also provides a means of assessing overall performance of the collection development program. A written collection policy can either be in print format, electronic format or both. Several reasons support the formulation and availability of a collection development policy in a  library  or  information  centre.  One  of  the  reasons  is  the  proliferation  of  electronic information  due  to  advances  in  information  communication  technology.  Collection development policy must be written or revised to include electronic resources as well. Another reason for having a written collection development policy is the problem of lack of continuity in both staff and funding. A written policy helps assure continuity and consistency in the collecting process despite changes in staff and funding. However, studies have shown that many information centres fail to formulate or update their collection development policies. One of the major reasons for this is because a good policy statement requires large quantities of data and a great deal of effort. A policy must change to reflect the changing community; therefore, collection development staff never finishes collecting data and thinking about the changes. 1.4 Collection Development Process Traditionally, the collection development practice in information centres involves planning, selection, purchase of new materials (acquisition), deselecting (weeding), and evaluation of the existing collection. 1.4.1 Planning Process The  planning  process  involves  determining  the  needs  of  the  users,  writing  collection development policies that guide the entire process of collection development, and setting aside a budget that will be used to acquire the materials. 1.4.1.1Budgeting Libraries and information centres use budgets to plan for future activities and to set various goals and objectives. The amount of money allocated each year for collection development determines the quality, quantity and effectiveness of any collection in an information centre. A budget is a plan of revenue and expenditure expressed in quantitative, usually monetary term, covering a specific period of time, usually one year. It is also regarded as a systematic plan for the utilization of manpower and material resources. With budgets, libraries and information  centres  are  able  set  specific  expectations  which  aid  in  evaluating  their performance throughout the year. Budgeting helps libraries and information centres to implement specific strategies to meet goals and objectives. 1.4.1.1 Budgeting Purposes Budget affects libraries in much the same way as they affect any organization. Typically, budgets serve three major purposes. These are: planning, coordinating and 1.4.1.2 Types of Budgets Lump- Sum Budget Typically, lump-sum budgeting involves the allocation by the library’s parent organization’s upper-level management of a “lump-sum” of budget resources to the library. The librarian is allotted a sum of money and does one’s best with that amount. The lump sum dictates the services and programs that can be provided, instead of the library defining the services and programs. The problem with this type of budget is that it is virtually impossible to relate a library’s lump-sum budget to the goals of the library. Since the lump-sum method lacks specific ties to corporate goals and objectives, many library managers prefer other types of budgets. Formula Budget When a library is funded through the formula budget, the budget allocation is typically tied to a numeric value such as number of students multiplied by an average amount of money allocated per student. This method however has the following weaknesses: the budget total is calculated at a late point in time and intrudes on advance planning – especially for purchases and staffing increases

COLLECTION MANAGEMENT NOTES Read Post »

Uncategorized

KCSE Past Papers 2018 Kiswahili Paper 3 (102/3)

Kenya Certificate of Secondary Education Kiswahili – Fasihi Karatasi ya 3 1.Lazima N ilreyaandika lâaaneno haya KWa lıiaba ya: Malrilioni wasio malazi Wabebao vifurushi vilivyo wazi wazungukao barabaranı bil a mavazi Milki yao ya ıraisha. Kwa niaba ya: Maelfu wanouawa bila haki wiki baada ya wiki leo sumu au spaki leo kamba au bunduki na kwa wale wanosubiri kunyongwa. Kwa niaba ya: Vijana walio mitaani wale mayatima wa maskini wazBngukao mapipani kila pembe mjini kuokota sumu kutia tumboni kujiua bila kujua ili kupata kuishi. Kwa niaba ya: Wakongwe wasiojiweza walao chakula kiłichooza wachuktiao choo wakijipakaza polepole wakijiangamiza katika vyumba vyao baridi na giza kwa sababu haWarla Watazama waga wauguza. Kwa niaba ya: waish i na nyingi hofu kwa sababu ya madawa tifutifu yatiwayo vyakulani yakitufanya wafu bila ya mtu kuona kama kwanba sote tu vipofu, Na kwa niaba yetu sote; Tuliofungwa vifungoni, duniani Tuliosukunıwa kingoni, maishani Tuliopokonywa maoni, machoni Tuliotiliwa sumu, malishoni Tuliodidimizwa kinyesini ili ‘maendeleo yaendelee kwenda njiani huku yakitema machicha ya roho zetu. (a) “Shairi hili linakatisha tamaa.” Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano saba kutoka kwenye shairi. ( alama 7) (b) Fafanua umuhimu wa aina mbili za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 4) (c) Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili. (i) tasfida (ii) kinaya (iii) tashihisi (alama 3) (d) Eleza kwa kutoa mfano, mbinu moja ambayo mshairi ametumia kutosheleza mahitajl ya kiarudh) katika ubeti wa tano. (alama 2) (e) Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari.(alama 2) (f) Bainisha nafsineni katika shairi hili.(alama 2) SEHEMU B: RIWAYA K. Walibora: Kidagaa Kimem›vozea Jibu swali la 2 au la 3. 2. “Riwaya hii ya aina yake inathibiiisha kwa usanii wa kupi8iwa mfano jinsi ndoto ya uhuru b wi Afrika imegeuka kuwa jinamizi.” (a) Eleza muktddhâ Wa dondoo hili. (alama 4) tb) Onyesha jinsi ndoto ya uhuru barani Afrika imegeuka kuwa jinamizi kwa kuwarejelea wahusika Wâftlâtâo: (¡) Majisifu (alama 8) (ii) Fao(alama 4) (iii) Wahudumu katika zahanati ya Nasaba Bora(alama 4) 3. (d) “Leo usukani uko mikononi mıvetu wenyewe. Mbeberu amekwisha ng ’olewa pamoja na mizizi yake.” Onyesha kinaya kalika kauli hii kwa kutoa mifano ku mi kutoka Kidagaa Kimemıvozea. (alama 10) (b) Tathmini mchango wa wanyonge katika kuzoroteka kwa hali ya maisha yao. (a lama 10)(alama 4) SEHEMU C: TAMTHILIA P. Kea: Kfgogo Jibu swali la 4 au la5. 4. Tusiwaruhusu watu wachache waliojazwa kasumba za kikoloni fiturejesha kwenye utumwa. Hatuwezi kukubali kutawaliwa kidhalimu tena!” (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) (b) Fafanua kinyume kinachojitokeza katika kauli iliyopigiwa mstari kwa kurejelea hoja kumi na sita kutoka kwenye tamthilia hii. ( alama 16) 5. “Si haki! Unayazika matumaini yetu. Unaifukia kesho yetu.” (a) Fafanua umuhimu wa mzungumzaji wa maneno haya katika kuijenga taınthilia ya Kigogo. (alama 6) (b) Kwa kurejelea hoja kumi na nne kutoka kwenye tamthilia, jadili namna uongozi wa Sagamoyo unavyoyazika matumaini ya raia. (alama 14) Sehemu D: Hadithi Fupi A. Chokocho na D. Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na Hadhithi Nyingine Jibu swali la 6 au la 7. Said A. Mohamed: “Tumbo Lisiloshiba” 6. “. . .lakini hakuiruhusu sahau îketi na kuitawala kichwan mwake. .. hapoi. .. Angepoaje na ule moto unaomlipukia kila mtu pale mtaani, umeacha mpaka sasa kOVu bichi moyoni mwa kila (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4) (b) Bainisha tamathali tatu za usemi ambazo zimetumiwa katika kauli hii. ( Fafanua sifa tano za mhusika anayerejelewa na kauli hii.(alama 3) (d) Huku ukijadili hoja nane, onyesha jinsi wakazi wa M adongoporomoka walivyolipukiwa na moto.(alama 5) 7. Onyesha jinsi maudhui ya utabaka yalivyoshughulikiwa katika Tumbo Lisiloshiba na Hadilhi Nvingine kwa kurejelea hadithi zifuatazo: (a) Mkubwa (alama 12) (b) Kidege (alama 8) Sehemu E:Fasihi Simulizi Soma utungo ufuatayo kisha ujibu maswali. Nalilitizama jua la kinjano Likijikokota kwa jitirnai kutBa Mbele ya nguu ya mlima uso kikomo likipisha machweo yenye giza la kaniki Likishindilia uzito wa nanga kwenye moyo tepetevu uloonja shubiri ya kwondokewa. Twalitazamana na hiyo shamsi ikipotelea kwenye upeo wa macho huku nyuma ikinambia “yamekwisha.”. Naliona kope zake zikimezwa na kiza Nikaliona jua likitoweka pamwe nawe Jagina wa maisha yangu. Nikaliona likikokota aushiyo likabwakura rohoyo kutoka kwenye vyangu vitanga. Kumbukizi zilikuleta kwenye jukwaa la akili yangu pazia likafunguka likayaleta mawio ya siku ya kvamkia kuuka kwako. Nalikuona kwenye ruya ukitazamana ana kwa ana na hasidi alokakawana kutuhasiri mi nawe Nalikiona kipaji chako kikitwaa wasiwasi ukawa ni kama wanywea kwa wake mtazamo. Hata uliponishika mkono kunambia tukimbile tuj‹ ponye nalikuwa rli mechelewa Ulikuwa keshanipa kisogo, huku nyuma waniita, “Mwanangu, njoo tujisalimishe Mwanangu njoo, nguvu zimenisha.” Kumbe hiyo ilikuwa tahadhari kWamba Iziraili yu karibu moyowe kuchukua? Kumbe wali ukisema,‘Buriani mwanagu?” Siku ya faradhi ilifika, mkono kulazimika kukupungia Naliutazama mwilio mtakatifu Nalilitazama tambolo liloumbuka wali uıredhibitiwa shujaa wangu ndani ya chumba chenye kuta na paa la mbao. Hata tulipokukaribisha, kwa lako kaburi Nilijipa kujiambia, “Hajenda popote mtiına bado wapiga.”v Nalirgoja unisalimu Nalingojea tabasamu lako lenye haya Ela hayo hayakutimila Walikuwa kesha kwenda Kuwa milki, ya ardhi isoshiba. Hata waliponena, “Udongo kwa udongo,” NiJikusitJa ewe yeli uso kifani ııkighani ubeti wa wimbo wako pendwa mawazoni mwangu, “Kifo ni hasidi, Ikiwa mimi Gunge Roho yarıgu nitamkabidhi Iziraili Mimi niliyekaidi bunduki ya Mzungu Katika kitali cha miaka minne Kwetu kukarudi fahari na jina. Mimi niliyeshindana na ndui na tetekuwanga, iliyow apukutislıa wana wote wa Ngome Nikabaki mimi, jogoo wa kijiji. “Kifo ni shujaa, Ikiwa mimi Gunge mwili wangu huu mtukufu kwa tambo na nemsi nitaukubalia kuwa lengo la dua za kuonewa imani kuwa karamu ya macho ya mahasimu kuvikwa suti na mwosha kufunikwa kwa udongo uliolaaniwa Mimi Gurige, Niliruhusu jabali kubwa Likibinye changu kichwa Likidhibiti ehangu kidari Linizibe zangu pumzi Girige niache kutawala.” Huu ni wimbo wa aina gani? (alama l) Andika sababu mbili kuthibitisha jibu lako la a(i). (alama 1) Ni nani anayeimbiwa na nafsineni? (alama 1) Bainisha matatizo eıawili yanayoikumba jamii inayosawiriwa na utungo buu. (alama 2) (iv) Bainisha mbinu zifuatazo katıka wimbo huu.(alama 2) (i) ritifaa (ii) mbinu rejeshi (iii). taashira (alama 3) Unanuia kutumia mbinu ya kutazama na kushiriki kufanya utafiti kuhusu nyimbo za aina hii. Eleza sababu sita za kuchagua mbinu

KCSE Past Papers 2018 Kiswahili Paper 3 (102/3) Read Post »

Uncategorized

KCSE Past Papers 2018 Kiswahili Paper 2 (102/2)

Kenya Certificate of Secondary Education Kiswahili UFAHAMU (Alama 15) Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. “Mabibi na mabwana, ndugu wapenzi, alianza Bi. Mkesha, “huu ni mwaka wa tano tangu tufanye uchaguzi mkuu uliowapa vigoda wenzetu hawa. Katika kipindi hiki kumetokea mengi ya kujipigia kidari, pametokea pia mengi, mengi mabaya ya kuitia jamii ya Tungama izara. Tumejipa mkono wa tahania kwa uteuzi wetu mzuri. Vilevile tumejisuta kwa uteuzi usio wa kuridhisha. Ndugu wapenzi, sina haja ya kuwakumbusha yote ambayo tumepitia; mmeyashuhudia yote. Ila ninayotaka kusema ni kwamba malengo yetu ya kuwateua viongozi yamesalitiwa. Ndugu zangu, itakumbukwa kwamba watangulizi wetu walianza safari ya kurejesha utu wa Mwafrika wakiwa na nia thabiti ya kuwabwaga maadui watatu wa maendeleo. Je, mnawajua maadui hao? Ni ujinga, magonjwa na umaskini. Waanzilishi wa taifa hili, pamoja na viongozi waliowafuata walipigania huduma za bure za afya, na elimu ya bure na ya lazima kwa wote. Vijana wetu walijitoma ugani kuzamia lulu ya elimu; wakaxidhihaki vitabu hadi kufikia kilelecha cha elimu. La kusikitisha ni kwamba elimu hii imekuwa laana kwao. Mnajua kisa na maana ya hali hii? Natija iliyotarajwa haikupatikana. Na haya si mageni kwetu. Mnajua wapo vijana humu vijijini ambao wamepiga lami kwa miaka na mikaka bila kuambulia kazi za hadhi ambazo waliahidiwa huko vyuoni. Hatimaye hawa hawa wenye shahada mbili, na wengine hata tatu, ndio wanaokuwa matarishi wa wale ambao walichechemea masomoni. Vijana wengine, kwa kukosa hata huo utarishi, wamearnua kuanzisha biashara rejareja ili kujikimu; wamekosa la mama, wanaamwa la mbwa. Sina haja ya kuwafafanulia kiini cha hali hii ya kutamausha. Ni dhahiri kwamba uthabiti wa taifa lolote lile hutegemea uthabiti wa uongozi, na uaminifu wa raia wake katika kuuwajibisha huo uongozi. Hata hivyo, inasikitisha kwamba wengi wetu tuinejipoka uwezo wa kuuwajibisha uongozi kwa kuwa mawindo rahisi ya uzungukaji mbuyu. Huu ndio uwele ambao umeufisidi utu wetu na kutusahaulisha thamani za kitaifa. Hebu niambie ewe mama mwenzangu, kuna faida gani kuuza kura yako kwa kibaba cha unga na noti ya shilingi mia moja, ati kwa kuwa unaambiwa, ‘Ukinichagua nitahakikisha kwamba ile Affirmative Action imezingatiwa? Ipo haja gani kuchomwa na jua ukiwafuata hawa hawa viongozi, ukiwaimbia nyimbo za kuwatia raia kichaa cha shangwe ili kuwapembeja wawapigie kura? Je, faida kwako imekuwa gani? Hujangojea kwa kipindi chote hiki kusakafiwa kwa hiyo barabara uliyoahidiwa siku ulipouza kura yako? Na ile ahadi ya ‘mwenzetu’ ya kuwaajiri vijana wetu kwenye Jeshi la Wanamaji imetimia? Hatujashuhudia watu wa akraba moja wakisombwa kutoka humu lcijijini kwenda kuchukua nyadhifa katika mashirika ya umma?” “Kweli waso hayawanamji wao, Bi. Mkesha amejikosha kweliweli,”Bi. Kuli alimwambia mwenzake Bi. Kengemeka kisha akaendelea.” Anatuambia yepi mageni ambayo masikio haya yangu yaliyokula chumvi ya miongo sita ushei ya miaka hayajasikia?” “Anasema tumpe nafasi ajitome kwenye uwanja wa majogoo,” akajibu Bi. Kengemelca, “atakuwaje tofauti na hao wanaurne?” Hata hao wanawake tumewahi kuwapa nafasi, wakatutenda zaidi ya wanaume. Usinikumbushe kura yangu niliyoipoteza kwa kumkweza Bi. Shali kwenye usukani. Siwezi kusahau namna ile ahadi ya maji ya mabomba na kuchimbwa kwa visima ilivyoishia kwenye kauli yake tu.” Tumetendwa sote mwenzangu,” alisema Bi. Kull, “inasikitisha kwamba dau ta masomo ya wanangu limeenda mrama huku nikikimlilia huyo huyo Bi. Shali. Kila mara tunasikia kupitia vyombo vya habari kwamba serikali imeanzisha Hazina ya Eneobunge kuyafadhili masomo ya watoto kutoka familia maskini. Lengo kuu, nasikia, ni kuhakikisha kwamba asilimia kubwa ya watoto haipati fursa ya kujiunga na shule tu, bali pia inakamilisha masomo ‘Hata hivyo, lıuu ni mwaka wa tatu tangu wanangu watatu waache masomo kutokana na ukosefu wa karo. Na „ usidhani ni karo ya shule ya kitaifa, la, hasha! Ni karo ya shule za kutwa ambapo niliwapeleka baada ya huyu huyu Bi.Shali kunitilia huku akinitolea huko kuhusiana na ufadhili wa masomo.” “Usinikumbushe yaliyomfika mwanangu Neema,” alisema Bi. Kengemeka huku akitwaa ukingo wa kanga yake kujipangusa machozi. “Mwana huyu alikaa nyumbani kwa muhula mzima,” akaendelea Bi. Kengenıeka,” dhiki ya kuwaona wenzake wakienda shuleni huku yeye anabaki nyumbani ikamfanya kuwa windo rahisi la mmoja wa hao wabunge, akaambulia uja uzito ambao hakuulalia wala kuuamkia. Mwenyewe mbunge ameshika hamsini zake kana kwamba hakufanya lolote. Mwanangu Jabali naye amehiari kuwa kibarua katika shamba la mbunge wa sasa. Mwenyewe anasema anataka kudunduiza pesa ili arudi shuleni kukamilisha mwaka wake wa mwisho. Na usidhani ni hao wangu tu waliofikwa na ya kuwafika. Tumewaona wana wa wenzetu tuliopiga foleni pamoja kuwateua hao hao wabunge, wakitumiwa kama masoko ya dawa za kulevya. Wengine wamegeuzwa walanguzi wa dawa hizi,” Bi. Kengemeka alikamilisha uzungumzi wake na kushusha pumzi kana kwamba ameutua mzigo mzito. Hata hotuba ya Bi. Mkesha ilipofikia ukingoni, Bi. Kuli alimwambia mwenzake, “Ninavyoona ni kwamba wanasiasa wote wamefınyangwa kutoka aina sawa ya udongo. Ikitokea kwamba tutampa huyu Bi. Mkesha kura, tumpe kwa kulazimika kikatiba kupiga kura; tusiwe na matarajio makuu. Inasikitisha kwamba vijana wetu waadilifu hawataki kujitia najisi kwa kuingilia siasa. Yule kijana wetu Angaza angekubali rai ya wazee kujitoma ukingoni tungemuunga mkono. (a) “Malengo yetu ya kuwateua viongozi yamesalitiwa.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hoja sita kutoka kwenye taarifa. (alama 6) (b) Eleza mchango wa wanyonge katika hali ya uongozi nchini Tungama. (alama 3) (c) Bainisha mbinu nne ambazo Bi. Mkesha anatumia kuishawishi hadhira yake. (alama 4) (d) (i) Andika kisawe cha, ‘kuwapembeja’ kwa mujibu wa taarifa. (ii) Andika maana ya, ‘amejikosha’ kulingana na taarifa. 2. UFUPISHO (Alama 15) Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Tangu jadi, jamii za Kiafrika zilikuwa na majukumu bayana ya kijinsia. Kila jamii ilipania kuyarithisha majukumu haya kwa vijana wa vizazi tofautitofauti. Katika jamii nyingi, vikao maalumu viliandaliwa ili kuwaelekeza vijana kuhusu namna ya kukabiliana na majukumu yao ya kijamii. Nyakati nyingine mafunzo haya yalitolewa katika vipindi vya burudani kama vile utambaji wa ngano. Kadhalika, maarifa ınengi kuhusu namna ya kukabaliana na majukumu na changamoto za jinsia mahususi yalitolewa kupitia sherehe maalumu za kitamaduni almaarufu miviga. Mifano ya sherehe hizi ni kama vile upashaji tohara, arusi, na hata matanga. Jamii za zamani, kama zilivyo za kisasa, zilikuwa na matarajio mahususi kwa watu wa jinsia zote. Mathalani, katikajamiinyingine zaKiakika, mwanamumendiye aliyetarajiwakuikimu aila yalıe. Katika kipindi cha Usasi na Kuhemera kwa mfano, mwanamume ndiye aliyekuwa na jukumu la kwenda

KCSE Past Papers 2018 Kiswahili Paper 2 (102/2) Read Post »

Uncategorized

KCSE Past Papers 2018 Kiswahili Paper 1 (102/1)

Kenya Certificate of Secondary Education Kiswahili – Insha 1. Lazima Wewe ni katibu wa chama cha Walinda mazingira Wasio na mipaka shuleni mwenu.Andika kumbukumbu za mkutano uliofanyika kujadili suala la uharibifti wa mazingira katika shuleni. 2. “Udanganyifu katika mitihani haumwathiri mwanafunzi tu, bali pia jamii yake.’ Fafanua. 3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya inethali ifuatayo: Mti mkuu ukigwa, wana wa ndege huyumba. 4. Tunga kisa kinachoanza kwa kauli ifuatayo: “Waja husema kuwa subira huvuta herr: hii yangu inazidi kuvuta machungu kila kuchapo. Hij herr itapatikana lini?” Tuama alijisemea kwa masikitiko.

KCSE Past Papers 2018 Kiswahili Paper 1 (102/1) Read Post »

Uncategorized

KCSE Past Papers 2019 Kiswahili Karatasi ya 3 (102/3)

Kenya Certificate of Secondary Education Kiswahili – Fasihi Karatasi ya 3 SEHEMU A: RIWAYA A. Matei: Chozi la Heri 1. Lazima (a) “Sasa haya ameyapa kisogo … kufunguliwa kwa kituo hiki ni kama mana iliyomdondokea kinywani kutoka mbinguni.” (i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) (ii) Bainisha tamathali mbili za usemi ambazo zimetumiwa katika dondoo hili. (alama 2) (iii) Fafanua umuhimu wa mhusika anayerejelewa katika dondoo hili katika kuijenga riwaya hii. (alama 6) (b) Jadili mikakati mwafaka ambayo vijana wanatumia kukabiliana na hali yao ya maisha kwa kuwarejelea wahusika wafuatao: (i) Chandachema (alama 4) (ii) Dick (alama 4) SEBEMU B: TAMTHILIA P. Kea: Kigogo Jibu swali la 2 au la 3 2. (a) Jadili mbinu kumi ambazo Wanasagamoyo wanatumia kupigana na utawala dhalimu. (alama 10) (b) Eleza jinsi mbinu rejeshi ilivyotumiwa kukuza vipengele vifuatavyo katika tamthilia hii. (i) Maudhui (alama 5) (ii) Wahusika (alama 5) 3. (a) “Ushahidi utatoka wapi kama kipanga ndiye hakimu kwenye kesi ya kuku?” (i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) (ii) Fafanua dhima ya vipengele viwili vya kimtindo vinavyobainika katika dondoo hili. (alama 4) (b) (i) Kwa kurejelea tamthilia jadili sifa sita za msemaji.(alama 6) (ii) Eleza umuhimu wa mandhari katika tamthilia hii. (alama 6) SEHEMU C: HADITHI FUPI Jibu swali la 4 au la 5 A. Chokocho na D. Kayanda (Wah): Tumbo Lisiloshiha na Hadithi Nyingine K. Walibora. “Nizikeni Papa Hapa” 4. (a) “Isije ikawa hapa habari ya kufuata asali ukafa mzingani.” “… Pana hasara gani nzi kufia kidondani?” (i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 5) (ii) Andika mbinu mbili za kimtindo zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 2) (b) Hadithi, Nizikeni Papa Hapa inahimiza uwajibikaji. Jadili.(alama 5) 5. (a) Onyesha jinsi unafiki unavyoshughulikiwa katika hadithi, “Shogake Dada ana Ndevu.” (alama 8) (b) Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo: (alama 12) “Bi. Hamida alitunga donge kifuani mwake. Na donge likaja juu. Likampanda na kumsakama kooni. Kweli? Uongo? Kweli au uongo yale maneno ya binti yake? Labda kweli anamfıkiria mambo mabaya binti yake tu. Labda kweli dhana yake ni mbovu. Bi. Hamida alichanganyikiwa na mambo. Alivutwa huku na huku na nafsi yake yenye chagizo. Upande mmoja sauti yake ya ndani ilikuwa inamtetea Safia, na upande wa pili wa nafsi yake ilikuwa ikimshuku Safia; na sauti zake zote mbili hizo zimo ndani ya kiwiliwili chake zinamvuta yeye mtu mmoja, Bi. Hamida. Hatimaye hakutambua afanye nini.” SEHEMU D: USHAIRI Jibu swali la 6 au la 7. 6.Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali Lilipo lile banda, lile pale, Kuna tuja kakonda, kwa uwele, Wala siye kupenda, hiyo ndwele, Ndwele ya kutishwa! Ni ndwele ya kutengwa, penye haki, Uwele wa kusutwa, pasi haki, Ugonjwa kupuuzwa, na miliki, Ndwele ya kutwishwa! Mwiliwe kawa sugu, viwandani, Uso una kunyugu, ziso fani, Ujira wake ndugu, ni mapeni, Ndwele ya kutwishwa! Na homa akipatwa, maishani, Kwa tiba apuuzwa, kama nyani, Hajulikani kuwa, yeye nani, Ndwele ya kutwishwa! Ana chawa nyweleni, ona dhiki, Na kunguni nguoni, ahiliki, Funza na miguuni, wamesaki, Ndwele ya kutwishwa! Bado yuasubiri, kisimati, Dhiki yake kutiri, ‘we tamati Ndipo iwe sururi, ya kidhati Nyota yake ni nyota ya huzuni. (K.Wamitila) (a) Fafanua kwa kutoa hoja sita kutoka kwenye shairi, jinsi nyota ya anayerejele wa ni ya huzuni. (alama 6) (b) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 6) (c) Bainisha aina zifuatazo za uhuru wa kishairi katika shairi: (alama 6) (i) inkisari (ii) kujifanyanga sarufi (d) Eleza tamthali tutu za usemi zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 3) (f) Eleza sifa mbili za anayelengwa katika shairi hili kwa kurejelea ubeti wa mwisho. (alama 2) (g) Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 2) 7. Soma Shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Kalma akili si mali, maskini na tajiri Wangalimoja sampuli, asikuwepo fakiri Na hangekuwa na mali, mwinyi bila kufikiri Kama akİlİ si mali, usingeweza fikiri. Ukeshapo kwa fikara, ni kwa wingi wa akili Kuwaza kigaragara, una mengi si kalili Na kuwa una tambara, metajirika kwa hili Kama akili si mali, usingeweza fikiri. Alokijenga kitanda, ana wingi wa akili Hata asiwe na bunda, hamithili kwa akili Hata naye paka nunda, pasipo akili hali Kama akili si mali, usingeweza fikiri. Akili kweli ni mali, kwa kuteua vya mwozo Singetumia akili, ungevila vya angamizo Afya ikawa thakili, na kuhiliki mawazo Kama akili si mali, usingeweza fikiri. Vipi gonjwa kikuganda, wawazia spitali? Huachi ukawa ng’onda, ukanyauka muwili Ugangani unakwenda, kutafuta afadhali, Kama akili si mali, usingeweza fikiri. Kama akili si mali, kusingekuwa na jela, Kuwatenga kuwa mbali, wenye hiana na hila, Kwa mbavu na ufidhuli, pamwe mbinu tolatola, Kama akili si mali, usingeweza fikiri. Tajiri na maskini wote wanayo akili, Ni kuwa hayafanani, waliyonayo makali Kabisa hawashibani, liwe lile au hili, Kama akili si mali, usingeweza fikiri. Kalma akili si mali, ‘singekuwa na hazina Ya kudadisi mithali, na kumpinga yako mnna Gani inadumu mali, kuliko huko kusana? Kama akili si mali, usingeweza fikiri. (T. Arege) (a) “Ufanisi wa binadamu hutegemea akili.” Fafanua kwa kurejelea hoja sita kutoka kwenye shairi hili. (alama 6) (b) Andika mifano ya vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili:(alama 4) (i) sitiari (ii) tanakuzi (iii) Swali la balagha (iv) kinaya (c) Eleza mbinu nne ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi. (alama 4) (d) Andika aina mbili za urudiaji zinazojitokeza katika shairi hili.(alama 2) (e) Fafanua muundo wa shairi hili.(alama 4) SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI 8. Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali. Shangazi anambila umewadia muda wa kukiacha kiambo cha Baba Nende kujinasibisha na ajinabi tusohusiana kwa ngeu wala usaha nache niwapendao nache aila nache matamanio ya elimu kufuatiya. Anambile shangazi Hino ni neema ela moyo wanirai “Wajitia shemere”, nami nauambia, “Najua si utashi wangu” ila hiari sina kwani lvii ni faradhi mitamba mepokelewa na ami kwa furaha kilobaki ni kuvuka kizingiti hiki.” Kwaheri’i Mama, kwaheri wanuna. (a) Ainisha wimbo huu kwa kuzingatia kipengele cha maudhui.(alama 2) (b) Andika sifa mbili za jamii inayosawiriwa na wimbo huu. (alama 2) (d) Unanuia kutumia mahojiano kukusanya habari kuhusu nyimbo za aina hii. (i) Eleza manufaa matano ya kutumia mbinu hii.(alama 5) (ii) Eleza changamoto tano za kutumia mbinu hii.(alama 5)  

KCSE Past Papers 2019 Kiswahili Karatasi ya 3 (102/3) Read Post »

Uncategorized

KCSE Past Papers 2019 Kiswahili Karatasi ya 2 (102/2)

Kenya Certificate of Secondary Education Kiswahili Karatasi ya 2 UFAHAMU (Alama 15) Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Kijiji chetu kilikuwa kimeanza kuingiwa na wasiwasi. Katika kipindi cha miaka michache iliyopita tulikuwa tumewapoteza watu kadha na hakuna aliyeelewa kiini hasa cha majanga haya. Wazee walisikika wakisemezana kwa sauti za chini. Hatukujua hasa walichosema lakini ilikuwa bayana kuwa kijui chetu kilikuwa juu ya mchongoma. Kuumi kwetu kuna mambo yatokeayo yakaonekana miujiza. Tunabaki kutapatapa kuelezea chanzo shake na wesemavyo, akili ni nywele kila mtu ana zake. Ila zipo nywele za koto na za singa. Lakini kuna watu wenye kuandamwa na tata, mti wowote uliokuwa karibu ulishikiliwa kwa tumaini la kuleta nafuu. Ndiyo, nafuu. Na ndivyo ilivyotokea kiasi cha kila mtu kuwa bingwa wa kufasiri asili ya janga na suluhu yake. Hali hii iliendelea mpaka walipofika wataalamu kuuini kwetu na kufanya utafiti wa kisayansi uliotufumbulia asili ya dhiki zetu. Siku hiyo ya kutolewa matokeo ya utafiti, kuul kizima kilijumuika kwenye uwanja wa shule mapema. Hakuna aliyeonyesha use wa furaha. Ilikuwa kama tuliokuwa mahakamani tunasubiri hukumu ya kesi ya jinai dhidi yetu. Siyakumbuki yote aliyosema yule mtaalamu lakini yapo yaliyotugusa sote. “Najua mna hamu ya kujua tatizo liko wapi. Kabla ya kulieleza tatizo lenyewe ningependa kusema poleni kwa misiba iliyowaandama. Kuwapoteza wapendwa si pigo kwa familia tu, bali pia kwa kuui na taifa. Na kuanzia sasa ninawaomba tushirikiane kuibadilisha hali hii. Hatuwezi kuendelea kuishi hivi,” alisema huku wanakuui wanamtazama kwa masikitiko makubwa. “Binadamu yumo katika awamu ya kujiangamiza”,aliendelea, “amefanya uvumbuzi wa teknolojia aali lakini ambayo sawa na mwaridi, ina miba. Miba hii sasa inamchoma kila aitundaye teknolojia. Kwa sababu ya wingi wetu, sasa tunataka kuzalisha mazao yetu haraka. Kwa sababu ya ongezeko kubwa la idadi ya watu walaji ni wengi lakini ardhi inazidi kujibana. Njia ya pekee ya kuongeza lishe ni kupitia uzalishaji zaidi wa vyakula. Katika ulimwengu ambapo vipando vile vile hurudiwa kupandwa kwenye ardhi ile ile, pato lake hupungua. Jibu la kuinua pato ni teknolojia. Teknolojia hii imebuni uzalishaji wa mbolea ya kemikali ambazo huchochea rotuba kwenye ardhi. Urutubishaji wa ardhi yetu ndogo umetuwezesha lcuzalisha chai, kahawa, mahindi na mazao mengine kwa wingi ili kukidhi haja yetu ya chakula. Zamani ardhi ilipokuwa kubwa na idadi ya watu ikawa ndogo, haja hii ya mbolea haikuwepo. Ardhi iliachwa kujirutubisha yenyewe. Madhara tuyaonayo sasa hayakuwepo wakati huo.” “Leo hii utashi wetu wa lcujitosheleza umetusukumizia ukingoni mwa maisha. Vyakula vyetu sasa vina kemikali hatari kutokana na mizizi ya mimea kufyonza virutubisho vyenye nitrojeni. Virutubisho hivi hustawisha mimea. Hata hivyo mimea hii tunayoila ina kemikali hatari kwa miili yetu. Kemikali hizi vilevile huingia kwenye nyasi ambazo huliwa na mifugo wetu. Mifugo hao hudhurika, nasi tunapofaidi bidhaa zao tunadhurika. Hata mito yetu na visima hupokea mikusanyiko ya kemikali hizi hatari, nasi tunazinywa kupitia kwa maji. Kemikali hizi husababisha saratani, na hili ndilo tatizo la kuut hiki.” Kauli hii ya mwisho iliutikisa umati ule. Sauti za wanaktjui zilisikika zikinong’onezana. Wengi wa wanakuut waliona kama kila kite pale kuutnt kilikuwa chanzo cha adhabu ya kifo kwao. Baada ya kule kutanabahishwa, ilisikika sauti ya mlevi mmoja aliyesema kwa sauti kubwa kabisa, “Ni hivi, ama tule hivyo vibaya tufe polepole au tuache kuvila tufe mara moja.” Tamko hili la mlevi liliwasisimua wote waliokuwa pale, wakapata walau sababu ya kucheka. Kucheka huku kuliwatia watu matumaini, wakaanza kuuliza maswali. Kwa nini mbolea itengenezwe kutokana na kemikali hatari? Hivi dunia haijui kuwa ipo hatari kwenye mbolea hizo? Je, waache kunywa maji na kutupa vyakula walivyokuwa navyo? Waliuliza maswali haya na mengine mengi. Yule mtaalamu hakuwa na mengi ya kusema kwa sababu alifahamu kuwa kila aina ya teknolojia ina faida na madhara yake. Kwa hivyo alieleza kwa ufupi. “Kemikali hizo ndizo huchochea rutuba ya ardhi ambayo huiwezesha mimea kukua na kutupa mazao mcnbi. Dunia inafahamu fika madhara ya kemikali zinazotumiwa kwenye mbolea lakini ifanyeje? Watu watakao kulishwa ni wengi. Ardhi imepungua kwa sababu ya wingi wa watu. watu wanataka kula ilhali ardhi hiyo ndogo haina tena rutuba. Hata maji hayo yaliyoathirika mtayanywa tu bado. Mtaishije bila maji Mtapika vipi? Mtakunywa nini? Hali hii tunaweza kuiondoa polepole kwa kuwekeza kwsnye ufugaji wa kuku, ng’ornbe na mbuzi wengi ili tutumie mbolea yao kurutubisha ardhi yetu. Wanasayansi wanasema itachukua yapata miaka mitano kuirejesha ardhi katika hali yake asilia.” Maelezo ya mtaalamu yule yalilta nafuu ya namna fulani kwa wanakijiji. Mzee mmoja alipewa nafasi kuzungumuza kabla ya kikao kufungwa. Mkutano ulipomalizika kijiji kilijua tatizo lilipokuwa na kuumaliza uvumi uliokuwa unaoteshwa kila leo. (a) Eleza sababu mbili za wanakijiji kuuona ugonjwa uliozuka kuwa miujiza.(alama 2) (b) Eleza madhara manne ya kemikali za mbolea kulingana na kifungu. (alama 4) (c) Bainisha mambo matatu yanayochochea kubuniwa kwa teknolojia mpya kwa mujibu wa kifungu. (alama 3) (d) Andika mambo mawili yanayoonyesha kuwa wazee wa jamii hii walikuwa na hadhi.(alama 2) (e) Fafanua maana ya ‘nywele za koto’ na ‘nywele za singa’ kwa kurejelea kifungu hiki (alama 2) (f) Kipe kifungu hiki anwani mwafaka (alama 2) 2. UFUPISHO (Alama 15) Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Demokrasia ya uwakilishi huweza kujitokeza kwa namııa tofautitofauti kutegeıvca ır‹atakwa ya nchi mahususi. Demokrasia ya Urais ni aina mojawapo ya demoloasia ya uwakilishi. Aina hii ya demokrasia humpa rais mamlaka makuu juu ya serikali. Rais huchaguliwa ama kwa njia ya rnojiı t.wa moja, au kwa kutumia wawakilishi. Yeye hawi tu kiongozi wa taifa, bali pia wa serikali kaına iliivyo Kenya, Marekani na Ajentina. Hali kadhalika, kuna Demokrasia ya Bunge. Aina hii huipa bunge mamlaka makubwa. Kitengo cha utekelezi cha serikali hupata mamlaka yake katika bungeni. Kiongozi wa taifa na kiongozi wa serikali huwa watu tofauti na wenye viwango tofauti vya mamlaka. Kwa kawaida, kiongozi wa serikali huwa na mamlaka makubwa zaidİ kama ilivyo Uingereza. Demokrasia ya kimabavu huelekea kupingana na dhana halisi ya deınokrasia. Katikaa demokrasia hii tabaka la juu pekee ndilo lenye haki ya kuchagua wawakilishİ Wa taifa. Umma lıauna lıaki hiyo. Mfano wa demokrasia hii ni Urusi. Demokrasia ina manufaa mengi. Demokrasia hulinda masilahi ya wananchi wote; si walio wengi, si walio wachache, si wenye nguvu, si wanyonge…Demokrasia pia husaidia kugatua mamlaka, lıivyo kuzuia kundi dogo

KCSE Past Papers 2019 Kiswahili Karatasi ya 2 (102/2) Read Post »

Scroll to Top